UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umeizidi kete klabu ya
Simba SC baada ya kumsajili kiungo kati wa timu ya Gormahia ya nchini
Kenya,Rama Saluma Mohamed aliyekuwa akiwaniwa na klabu hiyo.
Rama ametua kwenye klabu ya Coastal Union akitokea nchini Kenya
na kusaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo kwa kipindi cha mwaka
mmoja.
Rama aliyewahi kuichezea timu hiyo kwa mafanikio makubwa na kufanikiwa kupata namba kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya Harembee Stars alitua jijini Tanga juzi usiku akiwa na kulakiwa na viongozi wa klabu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya Klabuhiyo barabara 11,Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi amesemakikosi cha cha timu hiyo msimu ujao kinatarajiwa kuwa tishio kutokana na kufanya usajili wa nguvu ambao unaonekana utaleta upinzani mkubwa sana.Aidha amesema kikosi chetu msimu ujao kitakuwa tishio kwasababu tunamatumainimakubwa ya kufanya vizuri kutokana na usajiliimara ambao tumeufanya kwa kusajlili wachezaji nyota kama vile
Obina,Shabani Kado Sued Tumba ,Bakari Mtama, na wengine wengi walipokwenye kikosi cha timu hiyo Amesema bado wanaendelea na mchakato wa kuhakikisha wanaimarisha kikosi hicho kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara msimu ujao. (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment