Meneja wa Manchester United, Louis van Gaal amemsihi beki wake mpya  Marcos Rojo kupunguza ama kuacha kabisa tabia yake ya  ukorofi aliyo kuwa nayo akiwa huko Sporting Lisbon ya Ureno.

Vana Gaal: Ni lazima Rojo aache mambo yake ya ukorofi ili afurahie maisha yake katika ligi ya Uingereza.
Rojo ambaye amejiunga na Manchester United kwa ada ya Uro milioni 16 alikuwa mchezaji nyota wa kikosi cha Argentina  katika kombe la duniania 2014 huko nchini Brazili, lakini amejiunga na Mashetani Wekundu katikikati mwa Juma hili akiwa na rekodi mbaya ya ukorofi.

Kwa misimu miwili iliyopita akiwa katika klabu yake ya Sporting Lisbon,  Rojo alionyeshwa kadi ya manjano mara 15 na kadi  nyekundu mara 4. Yeye ndiye anayeshikilia rekodi ya kuonyeshwa kadi nyingi katika ligi ya "Portuguese Primera Liga"

Kwa kutambua hilo, bosi wa Mashetani Wekundu, Louis Van Gaal amemsisitiza beki huyo kurekebisha tabia yake hiyo ili aweze kufanya vizuri katika Ligi ya Uingereza.

(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top