Nahodha wa klabu ya Liverpool na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Steven Gerrard ameonyesha kukubali uteuzi wa mshambuliaji wa Manchester United , Wayne Rooney kuwa nahodha wa klabu hiyo akidai  kuwa  anaamimini Rooney anakipaji cha kuzaliwa cha uongozi.
 
"Kwa nini ninasema Wayne ni nahodha sahihi wa Man U?. Mbali na kuwa mchezaji mahiri uwanjani, pia Wayne ana kipaji cha uongozi, ni mtu mwenye uwezo wa kushawishi wachezaji wenzake ndani na nje ya dimba". Gerrard alisema.
 
Chilling out: Rooney (left) and Steven Gerrard relax during an England training session in the Algarve in May
Kwa upande wa kushoto ni Rooney, akiwa na Gerrard  kwa upande wa kulia wakiteta jambao walipokuwa kambini huko nchini Brazil wakati wa kombe la dunia 2014.
 
Mara nyingi Rooney amekuwa akizungumza na wachezaji wenzake kuhusi nini cha kufanya kabla ya mechi yoyoye hususani wanapokuwa katika vyumba vya kubadilishia nguo.

"Alipokuwa  msaidizi wangu katika timu ya taifa kiukweli alikuwa na mchango mkubwa sana siyo tu uwanjani lakini pia katika masula ya ushauri alikuwa anafanya vizuri sana". Gerrard aliendelea kusema.
 
Louis Van Gaal alimteua Wayne Rooney kuwa nahodha wa Mashetanini wiki moja kabla ya kuanza kwa ligi kuu ya Uingereza Agosti 16, 2014.
 
 
  (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top