Uongozi wa klabu ya Young Africans unasikitika kutangaza kifo cha
aliyekuwa Dereva wa Bus Kubwa la Wachezaji (Yutong) Bw Maulid Kiula
kilichotokea alfajiri ya leo Ilala jijini Dar es salaam.
Ukiachilia mbali changamoto za ajali alizokuwa akizipata, Maulidi pia alikuwa akivumilia changamoto zingine kama vile za gari lake kupigwa mawe na timu pinzani hasahasa Yanga inaposhinda.
Jamii ya soka nchini Tanzannia na hata nje ya Tanzania kamwe haitasahau mchango wako wa hali na mali uliyokuwa unatoa!
Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwa marehemu mtaa wa Chunya karibu na Bungoni Ilala jijini Dar es salaam.
Mungu ametoa, mungu ametwaa....PUMZIKA SALAMA!
0 comments:
Post a Comment