Mmoja wa wanakamati kuu ya utendaji ya shirikisho la kandanda duniani FIFA, Theo Zwanziger amesema hakuna uwezekano wa kombe la dunia mwaka 2022 kufanyika nchini Qatar katika miezi ya kawaida ya June na July kwa sababu ya kuwepo kwa joto kali sana miezi hiyo nchini humo.

kwa mujibu wa taarifa kutoka kitengo cha utabibu cha FIFA,unaonyesha kuwa kiwango cha joto nchini Qartar mwezi June na July hupanda hadi kufikia nyuzi joto 50, joto ambalo ni kali zaidi kwa binadamu wa kawaida kustahimili.
Zwanziger believes the extreme hot weather will make it impossible for FIFA to stage the tournament in Qatar
Theo Zwanziger

Licha ya serikali ya nchini Qatar kujigamba kwamba  ina uwezo wa kupooza hali ya joto katika viwanja vyote vitakavyokuwa vikitumika katika kombe la dunia 2022, Zwanziger ambaye pia ni muwakilishi wa nchi ya Ujerumani FIFA, aliendelea kuhoji juu ya usalama wa watu nje ya uwanja na joto hilo.

Theo Zwanziger alisema hata kama kuna uwezekano wa kupooza hali ya hewa ndani ya uwanja bado tatizo litaendelea kuwa palepale kwani nje ya uwanja joto litakuwa lilelile na ikumbukwe kwamba kutakuwa na watu kutoka mataifa mbalimbali watakao kuja kushuhudia mashindano hayo ambao ni wageni na mazingira ya Qatar.

Aidha, kuna taarifa kuwa wataalamu wa afya pia wamesema hawata husika na madhara yeyote yatakayo wapata watu nchini Qatar endepo FIFA italazamisha kombe la dunia 2022 kufanyika nchini humo.



(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top