“Kwa niaba ya mteja wetu, Emmanuel Arnold Okwi,napenda kutoa maelezo kuhusu Uamuzi wa
kihistoria katika soka la Tanzania ambaoumefanywa na Kamati ya Sheria na hadhi ya wachezaji ya TFF".
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni: Ni wazi kwamba kuna wachezaji wengi wa VPL, wananyanyasika katika klabu zao lakini wanaogpa kusema waziwazi, alichokifanya Okwi inaweza ikawa ni somo tosha wachezaji wengine |
Uamuzi huo ni wa kihistoria kwamisingi ifuatayo:
MOSI: Ni mara ya Kwanza katika historia ya sokala Tanzania ambapo Kamati inakaa kujadili haki ya
mchezaji dhidi ya klabu kubwa na hatimaye kuamua kwa manufaa ya mchezaji, tena pasipo
kupiga kura kwa misingi ya upenzi na unazi.Kamati ya Mwanasheria Mashuhuri na mwenye Msimamo Bw. Richard Sinamtwa iliamua kustafsiri kanuni kwa kufuata ushahidi uliopo na kwa haki
kabisa pasipo kujiingiza katika mtego wa kupiga kura kama ambavyo tumekua tukiiona huko
nyuma.
PILI: Kamati ikiongozwa na Mwenyekiti ilitumia busara ya hali ya juu kwa kukataa ombi la Yanga la
kutengua uteuzi wa Bw. Hans Pope katika Kamati hiyo. Ikumbukwe kuwa Yanga ilileta hoja ya
kumkataa Bw. Hans Pope kwa misingi ya mgongano wa kimaslahi na kumtaka mwenyekiti atoe uamuzi juu ya suala hilo. Endapo mwenyekiti angetoa maamuzi ya kumuondoa Hans Pope, basi
angejiingiza katika uvunjaji wa Katiba ya TFF kwasababu yeye sio mamlaka ya uteuzi wa Hans
Pope katika Kamati hiyo. Mwenye mamlaka hayo ni Kamati ya Utendaji ya TFF. Hivyo Yanga
walipaswa kuelewa hilo na si kuishinikiza kamati,hususan Mwenyekiti, amuondoe Hans Pope
kwenye Kikao.
TATU: Maamuzi ya Kamati yamefungua njia kwa wachezaji wengi ambao mikataba yao inachezewa
na vilabu kwa muda mrefu pasipo kuwa na nafuu yoyote ya kisheria kwa wachezaji hao ambao ndio
nguzo ya muhimu katika mpira wa Tanzania. Hata hivi sasa kuna wachezaji ambao bado hawajalipwa
stahili za mikataba yao ndani ya Yanga.Tunawaomba wajitokeze ili tuwasaidie wapate haki
zao za kisheria kama ambavyo imetokea kwa
Okwi.
NNE: Pamoja na madai ya Yanga ya kukata rufaa FIFA / CAS, naomba wajue kuwa haki yao ya
kukata rufaa inatokana na ukweli kuwa Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF imetekeleza
wajibu wake. Uamuzi huo wa Kamati umejenga msingi muhimu sana katika suala zima la kuheshimu na kutekeleza mikakaba kwa mujibu wa kanuni za FIFA. Endapo Yanga watakata rufaa kama wanavyodai, itakuwa ni hatua muhimu katika kuhakikisha nguzo ya kuheshimu mikataba ya
wachezaji inapewa msisitizo unaostahili.
MGOGORO KATI YA YANGA NA OKWI
Mkataba wa Yanga na Okwi, ambao ulisainiwa tarehe 12 Disemba 2014 umekuwa na mapungufu
yafuatayo:
1. Mkataba huo umempa majukumu mchezaji kufuatilia ITC na suala zima la yeye kupata vibali
vya kucheza. Hii ni kinyume na Kanuni za FIFA ambao zinatamka bayana kuwa jukumu la
kufuatilia ITC ni la wanachama wa FA, lakini Yanga walimtwisha Okwi zigo hilo. Okwi alitekeleza
jukumu hilo.Kamati ililiona hilo na kusema wazi kuwa hilo siosahihi. Ni vema wachezaji wajue kuwa hilo sio jukumu lao.
2. Pili Yanga, kwa mujibu wa mkataba, walikuwa na haki ya kumkata mchezaji theluthi moja ya
mshahara wake wa mwezi endapo atakosa mechi tatu au zaidi. Yanga walimkata Okwi Mishahara ya
miezi mitano, kinyume na matakwa ya mkataba na pasipo maelelzo yoyote.
3. Yanga na Okwi walikubaliana kuwa mchezaji atalipwa ada ya kusaini mkataba (signing on –
fee) ya US$ 100,000, kwa Awamu mbili. Awamu ya kwanza wakati wa kusaini mkataba na awamu
ya pili tarehe 27 Januari 2014. Mpaka hivi sasa,Yanga wamelipa US$ 50,000 tu na bado kuna deni
la US$ 50,000. Huu ni uvunjaji wa mkataba wa wazi kabisa.
4. Kipindi chote mchezaji akiwa na klabu ya Yanga,hajapewa nyumba kama ambayo walikubaliana.
Huu ni ukiukwaji mwingine wa mkataba.Baada ya Okwi kuanza kudai haki zake tajwa hapo
juu, Yanga waliamua kutomlipa mteja wetu mishahara ya miezi mitano kinyume na matakwa
ya mkataba kati yao.
MPANGO WA SIRI WA YANGA
Yanga walikuwa na mpango wa siri wa kuvunja mkataba na Emmanuel Okwi ili wamkomoe mteja
wetu, ashindwe kucheza mpira, kiwango chake kiporomoke na itumike kama onyo kwa wachezaji
wengine ambao wanadai haki zao. Mpango huu ulitekelezwe kama ifuatavyo:
a. Tarehe 27 Juni 2014, Yanga waliandika barua kwenda TFF, ikiitaka TFF, pamoja mambo mengine,
itambue kuwa mkataba kati yao na Okwi umefutwa. Barua hiyo haikuwa na nakala kwa
Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
b. Tarehe 25 Julai 2014, Yanga waliandika barua yapili kukumbushia barua yao ya tarehe 27 Juni 2014.Barua hiyo ya pili haikuwa na nakala kwa Okwi,ambaye ndiye upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.
c. Tarehe 20 Agosti 2014 Yanga waliandika barua nyingine tena wakikumbushia hoja zao tajwa hapo
juu. Kwa mara ya tatu, barua hiyo haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye upande wa pili wa
mkataba ambao unapaswa kufutwa.
d. Yanga waliandika barua nyingine ya nne tarehe 25 Agosti 2014 ikiwa na hoja zile zile za kusitisha
mkataba na mteja wetu. Kwa mara ya nne barua hiyo haikuwa na nakala kwa Okwi, ambaye ndiye
upande wa pili wa mkataba ambao unapaswa kufutwa.Baada ya TFF kupanga tarehe ya kikao cha Kamati ya Sheria na hadhi ya wachezaji na kutoa barua ya wito tarehe 27 Agosti 2014 ndipo kwa mara ya kwanza mchezaji Emmanuel Okwi akafahamu kuwa Yanga wameomba kuvunja mkataba wake.Tarehe 27 Agosti 2014, Emmanuel Okwi aliiandikiaYanga KUKUBALI ombi lao la kuvunja mkataba.Mambo muhimu ya kujiuliza ni:
Mosi, Kama Mkataba ulikuwa ni kati ya Yanga na Okwi, ni kitu gani kiliifanya Yanga ishindwe kumpa angalau nakala ya barua nne ambazo ilizipeleka
TFF?
Pili, Wakati Yanga wanaomba kuvunja mkataba,walikuwa wameshamlipa Okwi stahili zake kwa
mujibu wa Mkataba huo?
Tatu, Je visingizio vya kuvunjwa kwa mkataba wa Okwi vina uhusiano na idadi ya majina ya
wachezaji wa kigeni wa Yanga? Ni bayana kuwa Yanga walitafuta kila aina ya kisingizio ili mteja wetu aonekane kuwa ndio amevunja mkataba wakati ni wazi kuwa Yanga ndio waliokuwa wa kwanza kuvunja mkataba huo tarehe 27 Januari 2014 kwa kushindwa kumlipa
mteja wetu US$ 50,000 za ada ya kusaini mkataba.
HOJA MBELE YA KAMATI
Mbele ya Kamati Yanga walileta hoja kuwa: Hans Pope ana mgongano wa maslahi kwa kuwa
amemsajili Okwi Simba na yeye ni mjumbe wa Kamati hii; Okwi amekataa kuongeza au
kupunguza mkataba kama ilivyopendekezwa na Yanga; Okwi ameleta madai yasiyo na msingi ya
kutaka apewe nyumba ya kuishi; hajacheza mechi 6 hivyo kuikosesha Yanga ubingwa. Okwi
amefanya makubaliano na Klabu ya Wadi Geldi ya Misri wakati ana mkataba na Yanga. Hivyo basi
Yanga waliitaka Kamati itamke kuwa mkataba kati yao na Okwi umesitishwa, imfungie Okwi kucheza mpira Tanzania Maisha na ailipe Yanga dola za kimarekani laki mbili.Tukimwakilisha Okwi, tulitoa hoja kuwa: Mteja wetu amekubali ombi la Yanga la kuvunja mkataba ambalo limo katika barua zake nne; Yanga ndio wamevunja mkataba kwa kushindwa kulipa signing fee US$ 50,000; Mishahara ya miezi mitano US$ 15,000 na kodi ya nyumba US$ 2,800. Madai hayoni kwa mujibu wa mkataba.Baada ya Maswali toka kwa Kamati kwa pande zote mbili, Yanga waliomba kufuta barua zao, ombi ambalo lilitupiliwa mbali na kamati.Kamati, hatimaye ilifanya maamuzi ya kihistoria katika kulinda haki za kimkataba za wachezaji kama ambayo imeelezwa hapo juu. Kwa mtu yoyote mwenye akili timamu, anapaswa kuipongeza kwa dhati kamati kwa maamuzi ambayo wanajenga mpira wa nchi hii. Vilabu vinapaswa kufahamu kuwa haki za mchezaji
lazima ziheshimiwe. Hoja za Yanga kuwa hakukuwa na madai ya fedhasio sahihi kwasababu Majibu toka kwa Okwi na mabishano ya maneno mbele ya kamati hiyo ilijadili kwa kina madai ya fedha ya Okwi na hata Yanga walikiri kutolipa madai hayo. Hivyo basi si sahihi kusema kuwa eti suala la madai ya fedha halikujadiliwa. (ona kiambatisho MNA1) Msingi wa malalamiko ya Yanga ni barua ya tarehe27 Juni 2014, ambayo hakuna sehemu ambayo inatamka suala la Simba. Kama kuna kesi dhidi ya Simba, wasubiri wakati wa kupitia pingamizi za usajili lakini suala ambalo Yanga walilalamikia ni kusitisha mkataba na Okwi na madai ya fidia. Kamati ya Sheria na Mwenyekiti wake hawana mamlaka ya kujadili uteuzi au uwepo wa Hans Pope kwenye kikao hicho. Mamlaka ya Uteuzi ndio, kwa mujibu wa katiba ya TFF, yenye uwezo wa kutoa uamuzi kuhusu suala hilo.
Kwakuwa rufaa ni haki ya kila mtu, Uamuzi wa kukata rufaa Fifa / CAS ni haki ya kisheria lakini
tuwakumbushe Yanga kuwa “UKITAKA HAKI, TENDA HAKI KWANZA”.
“Imeandikwa na Dk. Damas Daniel Ndumnbaro
(PhD) wa kampuni ya Maleta & Ndumbaro
Advocates, ambao ni Mawakili wa Mchezaji
Emmanuel Okwi”
0 comments:
Post a Comment