![]() |
Uwezo aliokuwa anaonyesha jana Suarez uwanjani, ni faraja kubwa sana kwa kocha wa Barcelona FC, Luis Enrique ambaye anategemea kumtumia nyota huyo katika mechi ya El clasico ( Barcelona vs RealMadrid) Octoba 25, 2014 |
Luis Suarez alipigwa marufuku kushiriki mashindano yoyote kwa muda wa miezi minne pamoja na adhabu ya kutoshiriki mechi 9 za kimataifa baada ya kumg'ata beki wa timu ya taifa ya Italy, Giorgio Chiellini wakati wa michuano ya komba la dunia 2014. Adhabu zake zote zinatarajiwa kumalizika Octoba 25, 2014
Kwa upande mwingine, Giorgio Chiellini "kitoweo cha Suarez" jana alifungia timu yake ya taifa magoli 2-1 wakati ilipokuwa ikipepetana dhidi Azerbaijan. Chiellini ndiye amewasaidia Azerbaijan kupata goli baada ya kujifunga.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment