Tabia ya meneja wa Chelsea, Jose Mourinho ya kusaliamia/kupongeza makocha wa timu pinzani kabla ya mchezo kumalizika, inawakera watu wengi sana kwa kuwa wengi huamini ni hali ya madharau.
Keane: achana na huyo mshenzi kwani haoni mchezo bado unaendelea uwanjani. Hiyo ilikuwa ni mechi kati ya Chelsea dhidi Astone Villa Sep 27,2014, mchezo ambao ulimalizika kwa The Blues  kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 Stanford Bridge

Roy Keane, ambaye ni kiungo wa zamani wa klabu ya Man U na kocha msaidizi wa klabu ya Aton Villa kwa sasa, amekaririwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Uingereza akisema kwamba tabia ya Mourinho kuwapa mkono makocha wa timu pinzania kabla mechi haijamalizika, ni utovu wa nidhamu na kamwe haivumiliki.

"Nimekuwa nikimuona akifanya hivyo kwa makocha mbalimbali wa timu pinzania, hasa hasa pale anapokuwa anaongoza mchezo kwa magoli mengi. Anajifanya haoni kama mchezo bado unaendelea, mimi kwa kweli namwona kama ni mshenzi fulani" Keane alisema.

Mbali na hiyo, Roy Keane pia ametoa kitambu kinacho chambua kwa kina migogoro yake na aliyekuwa kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguso. Kitabu kinaitwa "Roy Keane Second Half"


(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top