Mpambano mkali wa mchezo wa masumbwi mkali utakaokutanisha mabondia mbalimbali kutoka kila kona ya Tanzania utafanyika October 25 katika ukumbi wa
friends Corner manzese jijini Dar es salaam akizingumza na waandishi wa
habari mratibu wa mpambano huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi
nchini Rajabu Mhamila 'Super D'amesema kuwa siku hiyo kutakuwa
na mpambano wa mahasimu katika mchezo wa ngumi kati ya bondia Saidi
Mbelwa 'Moto wa Gesi' na George Dimos mpambano mwingine utawakutanisha
Amani Bariki 'Manny Chuga' na Ally Bugingo mpambano unaosubiliwa kwa
hamu kila kona ya jiji la Dar es salaam ambapo mabondia hawo wamejizolea
umaarufu mkubwa kupitia mchezo huo
pambano jingine ni kati ya Juma Fundi atakaezichapa na Hamza Mchanjo wakati Hasani Mandula ataonyeshana kazi na Mohamedi Jaka na Shabani Kaoneka atazipiga na Ibrahimu Maokola anaejiandaa kuwania kucheza ubingwa wa taifa mwishoni mwa mwaka huu Fadhili Boika atazipiga na Godfrey Silver na Habibu Pengo atazidunda na Abdallah Luanje, Kashinde Mohamedi atazidunda na Mohamed Kibaga wakati Sadiki Nuru atakumbana na Mohamed Mbishi.
![]() |


0 comments:
Post a Comment