
Ozil alikiwa ni sehemu ya kikosi cha Ujerumani, mabingwa wa kombe la dunia msimu uliopita, ambao walikuwa wanajiandaa kukipiga dhidi ya Poland na baadaye Jamuhuri ya Iland kuwania tiketi za kushiriki fainali za mataifa ya Ulaya ya 2016, lakini ndoto zake za kuendelea kuwa sehemu ya kikosi hicho zinaonekena kufifia kwa sababu ya majeraha hayo ambayo mpaka sasa haijawekwa bayana kwamba itamuweka nje ya dimba kwa muda gani.
Hili pia linaweza kumpa Arsene Wenger presha, kwa kuwa Ozil ni mmoja kati ya wacheza wanao wategemea sana kikosini hapo kwa sasa baada ya kuwa na idadi kubwa ya majeruhi mapema kabisa msimu huu. Wachezaji wengine ambao ni majeruhi katika klabu ya Arsenal mbali na Mesut Ozil ni; Olivia Giroud, Mathieu Debuchy Aron Ramsey, Mikel Arteta pamoja naye Theo Walcott ingawaje baahi yao wanaweza kurudi uwanjani muda mfupi.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment