![]() |
| Baloteli akipambana na mchezaji wa QPR, Richard Dunne katika mechi ya jana. |
Licha ya jana Liverpool kushinda kwa jumla ya magoli 3-2 dhidi ya Queen Spark Rangers katika dimba la ugenini Loftus Road Studium bado wadau na mashabiki wa Liverpool wameendelea kumuandama mshambuliaji wao, Mario Baloteli kwa kushindwa kufunga hata goli moja katika mechi hiyo.
Lakini, meneja wa Liverpool yeye alikuwa na mtazamo wa tofauti kabisa na wadau hao wanao mlaumu Baloteli kwa kushindwa kuonyesha makeke kama ambavyo wengi walikuwa wakitegemea.
"Nafahamu kiwango cha Baloteli cha kufunga magoli mengi kitapanda muda wowote, nachoshukuru ni kwamba kiwango cha Baloteli cha uwajibikaji uwanjani ni cha kuridhisha licha ya kwamba hana bahati ya kufunga magoli.
Baloteli amefanikiwa kufunga goli moja tu katika mechi tisa alizocheza tangu ajiunge na Liverpool msinu huu kwa ada ya pauni milioni 16. (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:
Post a Comment