Moyes hakuwahi kupata kazi nyingine tena tangu afukuzwe Man U kwa sababu ya matokeo mabovu katika klabu hiyo msimu uliopita. 
Baada ya klabu ya Real Sociedad kumtimua kocha wao Jagoba Arrasate Jumapili iliyopita kwa sababu ya matokeo mabovu yaliayo iandama klabu hiyo tangu kuanza kwa ligi kuu nchini Hispani msimu wa 2014/15, jina la kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United, David William Moyes limekuwa miongoni mwa majina yanayopewa kipaumbele kujaza nafasi hiyo ambayo ni wazi kwa sasa.

Rais wa Real Sociedad Jokin Aperribay, amethibitisha  kwamba tayari uongozi wa klabu hiyo una majina ya makocha takribani wanne kutoka sehemu mbalimbli ambao wanawachunguza uwezo wao kuona ni yupi anafaa kuridhi mikoba ya kocha wa Arrasate.

"Majina mengi yametajwa katika mkutano kuhusu nani wa kuridhi mikoba ya Jagoba Arrasate, niweke tu wazi kwamba ni kweli tayari tumeshazungumza na kocha Pepe Mel pamoja na David Moyes kuhu kazi hiyo lakini bado tunawasiliana na makocha wengine ambao wako tayari kuwania nafasi hiyo".alisema Aperribay.

Tangu kuanza kwa ligi kuu nchini Hispanai, klabu ya Real Sociedad imefanikiwa kushinda mechi moja pekee kati ya mechi 10 alizocheza.




(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top