Baada ya mchakato mrefu, klabu ya Real Sociedad ya Hispania imempatia kocha wa zamani wa Manchester United, David Moyes mkataba wa mwaka mmoja na nusu kuinoa klabu hiyo baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Jagoba Arrasate kutupiwa virago wiki chache zilizopita.

Moyes hakuwa na kibarua chocote tangu akatishwe mkataba wake kunako Oldtraford mwezi April msimu uliopita kwa sababu ya matokeo finyu yaliyo iandama klabu hiyo tangu aridhi kazi hiyo kutoka kwa Alex Ferguson.

Tangu ligi kuu nchini Hispania imeanza, timu ya Real Sociedad imefanikiwa kushinda mechi mbili kati ya mechi 11, walizozicheza.

Kwa sasa klabu ya Real Sociedad ipo katika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Laliga, ikiwa imejikusanyia alama 9 pekee. Ujio wa Moyes unategemewa kuleta mapinduzi makubwa yatakayo ifanya timu hiyo kupanda juu kutoka karibu na msitari mbaya wa kushuka daraja.



(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top