Katika mchezo huo ambao Uholanzi iliibuka na ushindi mzito wa magoli 6-0, Blind, alishuhudiwa akitoka nje ya dimba katika ya dakika ya 20 ya mpepetano huo baada ya kugongona bahati mbaya na mchezaji wa Latvia, Eduardas Visnakovs.
Hali hiyo inampa wakati mgumu meneja wa Mashetani Wekundu, Louis Van Gaal kuelekea katika mchezo wa Jumamosi ijayo dhidi ya Arsenal kwa kuwa wachezaji waote walioumia ni wa kikosi cha kwanza. Kwa sasa Man U wapo katika nafasi ya saba, alama moja nyuma ya wapinzani wao Arsenal ambao tayari wamesha kusanya alama 17 tangu ligi ianze.
Mbali na Daley Blind, wachezaji wengine wa Man U walioko nje ya dimba kwa sababu ya majeruhi ni; Mlinda lango David Gea pamoja Michael Carrick.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment