Maka Malwisyi upande wa kushoto akiwa katika mahojiano maalum na mwandishi wa michezo Mlimani TV , Khalid Msabaha. |
Katika ligi hiyo; timu za Mwadui Fc ya Shinyanga, Majimaji Fc ya Songea, African Sports ya Tanga pamoja Toto Africans ndizo zilizo fanikiwa kupanda ligi kuu.
Akizungumza katika mahojiano maalum na mtandao huu, kocha mkuu wa Panone Fc ya mkoani Kilimanjaro inayoshiriki ligi daraja la kwanza, Maka Malwisyi amefafanua wazi kuwa ili uwe na uhakika wa kupanda ligi kuu kutoka ligi daraja la kwanza nchini Tanzania ni lazima ujue na uweze kucheza michezo yote ya fitina ikiwemo kuwahonga waamuzi na hata wacheza wa timu pinzana kama inawezekana.
"Mambo ya ligi daraja la kwanza ni magumu sana, hakuna mtu anayefuata sheria za mashindano hata kidogo. Ukienda kucheza ugenini ujue umefungwa, hivyo ndivyo mambo yalivyopangwa.
Nakuambia kati ya hizo timu nne zilizopanda ligi kuu msimu huu, nyingi hazikupanda kwa haki, na kama haki ingefuatwa basi si ajabu ni timu zingine tofauti na hizo ndiyo zingepanda ligi kuu", Malwisyi alisema.
Kocha huyo ambaye pia asili yake ni jijini Mbeya, ameshauri shirikisho la kandanda nchinTanzania TFF kuwa na utaratibu wa kurekodi mechi za ligi daraja la kwanza ili kuweza kufuatilia baadaye na kutoa maamuzi sahihi kwani hili litasaidia kutenda hakia kwa kiasi fulani.
Mbali na hayo, Maka Malwisyi pia amezungumzia hali ya mwenendo wa klabu yake ya zamani ya Mbeya City katika ligi kuu Tanzania bara ambapo amesema haridhishwi kabisa na kiwango kinacho onyeshwa na timu hiyo kwa sasa katika ligi kuu.
"Kwa kweli ukijaribu kuangalia Mbeya City ya msimu huu siyo ile Mbeya City ya msimu uliopita. Timu imebadilika sana hususani uwanjani, Mbeya City sasa hivi haina uhakika wa ushindi hata kidogo siyo uwanja wa nyumbani wala uwanja wa ugenini.
"Nafikiri kitu kikubwa kinacho sababisha hali hii ni wapinzani wa Mbeya City kutambua mbinu za Mbeya City. Ujue msimu uliopita timu nyingi za ligi kuu hazikuwa zikitufahamu kwa undani tofauti na sasa, kwa hiyo ilikuwa ni ngumu kwao kujua namna ya kujipanga kutuzuia na ndio maana tulikuwa tunawafunga kirahisi. Alisema Maka Mwalwisiyi.
Hivi karibuni Mbeya City ilipigwa magoli 3-1 na Yanga uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, kitendo kilichosababisha mlinda lango wa klabu hiyo David Buruhani kusimamishwa na uongozi wa Mbeya City Fc kwa tuhuma za hujuma. Uongozi wa Mbeya City Fc waliona kuwa magoli yote aliyofungwa goli kipa wao ni ya uzambe wake mwenyewe na ndiyo maana wakaamua kumsimamisha mpaka pale uchunguzi utakapo kamilika.
Maka Malwisyi kwa upande wake amesema hajaona makaosa ya kizembe yaliyofanywa na mlinda lango huyo.
"Ukiangalia magoli aliyofungwa David Buruhani, huwezi kusema ni uzembe wake kwa sababu mabeki hawakuwa wakitimiza wajibu wao ipasavyo. Angalia washambuliaji wa Yanga akiwemo Saimon Msuva, walivyokuwa wanacheza huru huku mabeki wa Mbeya City wakishindwa kuwa kaba kabisa na ndiyo maana goli kipa alikuwa akifungwa kirahisi.
Goli alilofunga Ngasa, makosa yalianzia kwa mabeki wa kati, beki alirudisha mpira nyuma pasipo na sababu yoyote wakati eneo lao halikuwa salama. Isingekuwa rahisi kwa Buruhani kuchezo ule mpira moja kwa moja bila kupiga chenga kidogo ile apate balance. Kwa bahati mbaya Buruhani amejaribu kupiga chenga lakini Ngasa kamzidi kasi na hatimaye akafunga goli, hayo siyo makosa mlinda lako peke yake bali ni ya safu ya ulinzi kwa ujumla", Malwisyi alisema.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:
Post a Comment