Fainali kati ya Nigeria-Burkina Faso kuchezwa kwenye uwanja wa nyasi bandia.

Hatimaye uwanja wa taifa ambayo michuano ya fainali za Afcon zitafanyikia Jumapili huko South Africa kutengenezwa kwa matirio bandia ili kuwezesha shughluli zingine mbali na michezo ya mpira wa miguu.
Fainali za Jumapili ya  Africa Cup of Nations  kati ya  Nigeria na Burkina Faso yanatarajiwa kuchezwa kwenye nyasi bandia ya uwanja wa Taifa maarufu kama  Soccer City.
 Soccer City iliyojengwa  2010 kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia  huku ikiwa na uwezo wa kuchukua watu 94,736, hivi sasa imefayiwa marekebisho ya hapa na palea ili kuwezesha shughuli zingine tofauti na soka kama vile muziki.
“Tumeamua kupanua uwanja tangu katikati ya mwezi Desembea mwishoni mwa mwaka jana na pia kubadilsha majani yake kuwa ya bandi kwa asilimia 50,” afisa alisema. “Tunasikia raha kwa asilimia 100 kwa kuwa uwanja umekidhi viwango vya FIFA. "Ninaamini ni miongoni mwa viwanja bora kabisa humu nchini kwa sasa.”
Wiki iliyopita ,bendi ya muziki kutoka Marekani Hot Red Chilli ilipata fursa ya kufanya shoo katika uwanja huo.
chanzo BBC.





(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top