Mlimani radio April 13, 2013
MAN CITY.
| MANCINI |
Wakati MANCHESTER CITY wakikabiliwa na kibarua kigumu hapo
kesho watakapo kutana na watoto wa darajani the blues,meneja wa klabu ya Manchester city ROBERTO MANCINI amekiri kukata tamaa ya kunyakua ubingwa wa ligi kuu nchini
UINGEREZA.
Manchini
ameendelea kusema kuwa licha ushindi wa magoli 2-1 waliopata dhidi ya
MAN U uwanjani OLDTRAFORD siku chache
zilizopita , anaamini tofauti ya gepu la point 12 linalowatenganisha mahasimu hao wa jadi kwenye ligi kuu nchini uingereza ni kubwa mno na amenyanyua mikono kwa hilo.
Meneja huyo ameongeza kuwa licha ya changamoto hiyo, wamejipanga kupambana kufa na kupona kwenye mchezo utakaopigwa kati yao na CHELSEA jumapili hii dimbani
WEMBLEY.
REAL MADRID.
| Mourinho. |
Ikiwa ni siku moja tu baada ya
shirikisho la mpira wa miguu barani ulaya, EUFA kutoa ratiba ya nusu fainali ya
michuano ya klabu bingwa barani ulaya,ambapo Vijana wa Jose Mourinho watakipiga
dhidi ya BORUSIA DORTMUND, huku BAYERN
MUNICH wakikabiliana na miamba ya soka ya uhispania klabu ya FC BARCELONA.
Kocha wa klabu ya REAL MADRID JOSE Mourinho amefunguka kwa kiungo wa zamani
wa timu ya taifa ya Ugerumani anayekipiga kwa sasa katika klabu ya BORUSSIA DORMUND,
STEFAN EFFENBERG, na kusema kuwa DORTMUND
ni timu ngumu sana kwake hivyo hataibeza hata kidogo.
EFFENBERG,
amesema kuwa siku chache wakati wakibadilishana mawazo na kocha huyo, amemkariri
akiweka wazi kuwa DORTMUND ni miongoni mwa
timu ngumu zinazomfikirisha sana, na amekuwa akijiandaa vilivyo ili
kukabiliana nayo.
Katika
hatua ya makundi borrusia dortmund ilijikuta ikijinyakulia pointi nne mbele ya
mabingwa hao watetezi wa kombe la ligi kuu nchini Hispania real MADRID, baada ya kuwachapa magoli 2-1 uwanjani SIGNAL IDUNA
PARK, Lakini vile vile wakitoka sare ya magoli 2-2 kwenye mtanange wakurudiana
uliopigwa dimbani SANTIAGO BERNABEU.
LIVERPOOL.
Suarez mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akihusishwa na tetesi za kuihama klabu ya Liverpool chini kocha BRENDAN RODGERS mapema msimu ujao licha ya kuifungia klabu hiyo magoli 22 kweye michezo ya ligi kuu nchini UINGEREZA.
Lakini Carragher, ambaye anatarajia kustaafu soka mwishoni mwa msimu huu, amesisitiza kuwa anamini kutokana na umuhimu wa SUAREZ klabuni hapo ataendelea kubaki licha ya klabu yake kupoteza matumaini ya kunyakua ubingwa kwa mara nyingine tena msimu huu.
Francis Kivuyo
Frank Momanyi Goal.com
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment