Wakati bodi ya vinara wap ya
wa ligi kuu nchini Uingereza, klabu
ya Manchester United hapo jana wakimthibitisha kocha wa Evaton, David Moyes kuridhi mikoba
ya Sir Alex Furguson mwanzoni mwa mwezi Julai, Mshambuliaji Wayne Rooney ametangaza kuihama klabu ya Manchester United muda wowote kwanzia sasa.
![]() |
Wayne Roony |
Rooney mwenye umri wa
miaka 27 akiongea kupitia mtandao wa klabu yake amesema miongoni mwa sababu
kubwa zilizomfanya kutangaza nia ya kuondoka klabuni hapo ni utofauti mkubwa wa
muda mrefu ulioko kati yake na meneja wa
huyo wa Evaton, David Moyes
aliyetangazwa rasmi kuridhi mikoba ya Furguson mapema mwishoni mwa msimu huu.
Lakini baada ya taarifa hizo kuenea katika vyombo mbalimbali vya habari, klabu
ya PSG, Chelsea, Beyern Munich pamoja nao Arsenal wameripotiwa kuingia katika
kinyang’anyiro cha kumsajili nyota huo.
![]() |
katuni ya mzee mzima Rooney ikionyesha timu zinazo mgombani |
Hata hivyo licha ya Rooney
ambaye anaingiza kitita cha mshahara
wa pound milioni 200 kwa wiki kutanganza
nia ya kuondoka klabuni hapo, Sir Alex Furguson amesisitza kuwa klabu yake haipo
tayari kumuuza nyota huyo.
FIFA
Shirikisho la mpira wa miguu duniani
FIFA , mapema leo hii wameeleza kuguswa na sababu zilizofanya mechi ya awamu ya
pili ya majaribio katika uwanja wa
Marakana uliko jijini Rio De Janeiro Nchini Brazil kushindwa kufanikiwa kwa sababu ya marekebisho
yanayoendelea uwanjani hapo.
![]() |
Dimba la Maracana |
Licha ya mchezo wa kwanza wa majaribio
kufanyika dimbani Marakana mwishoni mwa
mwezi Aprili mwaka huu mbele ya mashabiki 25000, uwanja huo umebainika kujengwa
kinyume cha maagizo ya FIFA baada ya dimba hilo kusababisha mashabiki kuleta vurugu kwenye maonyesho ya
mchezo huo.
Uwanja wa Marakana umegundulika
kujengwa kwa kufuata mtindo wa zamani tofauti na maagizo ya FIFA ambapo mashabiki
wanaokaa benchi nne za mwanzo uwanjani
hawawezi kutanzama uwanja vizuri kwa kuwa mabenchi hayo yako chini.
Kwa muji wa FIFA viwanja vyote sita nchin Brazil ikiwemo Maracana ambayo michuano ya kombe la mabara mwaka huu
na kombe la dunia 2014 yanatarajiwa kufanyika yametakiwa kurekebishwa upya kwa kufuata
taratibu mpya zilizowekwa na chombo hicho
Lakini uwongozi wa michezo nchini Brazil wamesisitiza kuwa
wanafanya kila liwezekana kurekebisha viwanja hivyo haraka iwezekanavyo kwa ajili michuano hiyo inayo kuja.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment