Kocha wa  zamani wa klabu ya Chelsea ameteuliwa  kuwa mridhi wa mikoba ya aliyekuwa kocha wa klabu ya Napoli,Walter Mazzarri  baada ya kocha huyo kutimukia kunako klabu ya Intermillan.
Rafael Benitez: Will return to Serie A as coach of Napoli
Rafael Benitez
Muhispania huyo alieondoka dimbani Stamford Bridge baada ya kandarasi yake ya  miezi sita kama kocha wa muda katika klabu ya Chelsea kufika tamati, na sasa ni kocha mkuu katika dimba la Stadio San Paolo msimu huu.
Kwa upande wake Benitez amesema anafurahia sana kupata fursa hiyo katika  klabu ya Napoli ambayo ni miongoni mwa vilabu vikubwa nchini Italy.

Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii, rais wa klabu  ya Napoli  Aurelio De Laurentiis siku ya Jumatatu jioni alli-tweet picha zinazomuonyesha akipeana mikono na Benitez ishara ya dalili ya kukamilika kwa  dili hilo, ambapo pia kwenye akaunt yake ya twitter aliandika hivi "Rafael Benitez ni kocha mpya wa klabu ya Napoli,ni mtu mkubwa mwenye uzoefu wa kimataifa lakini pia ni Kiongozi."
 Aurelio de Laurentiis
 
Kutoka kushoto, Rafael Benitez  na Aurelio De Laurentiis kwenye hoteli moja huko jijini London.

Benitez ameiwezesha klabu yake ya Chelsea kuchukua kombe la Europa League  lakini pia ameiacha klabu hiyo ikiwa katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu ya nchini Uingereza baada ya kuridhi mikoba ya aliyekuwa kocha mkuu klabuni hapo Roberto Di Matteo mwezi  November mwaka jana.

Mazzarri akiwa na klabu ya Napoli amenyakuwa kombe la Coppa Italia  2012 lakini pia ameiacha klabu hiyo ikiwa katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu nchini Italy. Miongoni mwa changamoto alizonazo Benitez katka klabu yake mpya ya Napoli ni kuhakikisha nyota wa klabu hiyo  Edinson Cavani haondoki baada ya kuwepo kwa tetesi nyingi kuwa nyota huyo ataondoka nchini Italy mwishoni mwa msimu huu. (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top