Wakisherehekea ushidi wa kombe la mabara dhidi ya timu ya Hispania Kocha wa wa timu ya taifa ya Brazilili, Luiz Felipe Scholari amesema kwa sasa juhudi zao nyingi wanawekeza kwenye maandalizi ya kueleke kombe la dunia 2014 litakalo fanyika nchini humo
 |
Kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Luiz Felipe Scholari |
Brazili ilifanikiwa kuiadhibu timu ya taifa ya Hispania kwa mabao 3-0 kuptia mshambuliaji Fred na Neymar kwa nyakati tofauti na kuifanya Brazili kuweka historia ya kuchukuwa kombe hilo mara tatu mfululizo na mara nne kwa ujumla
 |
Wachezaji wa timu ya taifa wakifurahia ushindi wao dhidi ya Hispania |
Lakini kufuatia kombe la dunia la mwaka 2014 linaloitarajiwa kufanyika nchini Brazili katka dimba la Maracana, Scolari anaamini timu yake itaendeleza kasi hiyo walioitumia katika kombe la mabara ili kuhakikisha wananyakuwa ubingwa huo
Hata hivyo kocha huyo alikwenda mbali kwa kusema kuwa binafsi anawashukuwa mashabaki waliokuwa ndani na nje ya uwanja kwa ushirikiano waliouonyesha kwa timu ya taifa ya Brazili
 |
Neymar |
Na nguli wa soka katika klabu ya Manchester United Wayne Rooney amekuwa akishawishiwa na mchezaji mpya wa msimu huu wa klabu ya Barcelona Neymar kujiunga na klabu hiyo katika kipindi hiki ambacho Rooney amekuwa akiandamwa na tetesi za kuihama klabu ya Mashetani wekundu kufuatia ujio wa kocha wa Everton David Moyes klbuni hapo
Akiwa amebakisha kandarasi ya miaka miwili na klabu ya Man U, Rooney aliomba uhamisho kutoka uongozi wa klabu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita lakini hakufanikiwa kitendo kilichofanya Barcelona hivi karibuni kutangaza dau la £25million huku Real Madrid and Chelsea wakimuhitaji nyota huyo pia.
 |
Mwenye mpira ni Rooney akiwa mazoezini na wachezaji wenzake. |
Hata hivyo habari za jana Jumapili zinasema kuwa nyota huyo wa zamani wa klabu ya Everton amefanya mazungumzo ya siri na kocha wake mpya klabuni hapo David Moyes ambapo inadaiwa alisema yuko tayari kubaki dimbani Oldtrafford endapo klabu hiyo itampa kandarasi yenye kulipa hela saw na kandasi yake ya sasa.
Neymar aliongeza kwa kusema kuwa anamshauri Rooney kufuata nyayo zake na kujiunga na klabu ya kubwa ya Fc Barcelona
"Kutokana na style ya football ambayo Barcelona inacheza na kiwango cha wachezaji tulionao - sisi ni klabu halali kwa wachezaji wakubwa kujiunga". Neymar alisema
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment