Onjaoftian Sokoni One, Arusha.
Mtu anayedaiwa kuwa jambazi sugu, Lembris Taiko (Doctor Mbushii) anayeyekadiriwa kuwa na miaka kati ya 30 na 35 mkazi wa Sokoni One ameua na jeshi la polisi jana jijini Arusha wakati wa majibizano wa risasi na polisi wakati polisi hao wakijaribu kumtia mbaroni.

Akiongea na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema kabla ya tukio hilo, majira ya saa moja usiku, poplisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kulikuwa na watu watatu wanasodakiwa kuwa ni majambazi katka eneo la Ojaftian Sokoni One na ndipo jeshi la polisi mkoa likatuma askari wake katika eneo la tukio ambapo walifanikiwa kuzingira nyuma alimokuwemo jambazi huyo na kuamuru watu wote waliokuwemo humo kujisalimisha lakini jambazi huyo alianza kuwalenga askari hao kwa risasi ambapo askari walijibu mashabulizi na kufanikiwa kumuua
Kamanda wa polisi Arusha, Liberutus Sabas
Silaha aliyokutwa nayo jambazi huyo.
Baada ya jeshi lapolisi kufanikiwa kuingia ndani ya nyuma hiyo aliyokuwemo jambazi huyo, walikuta Bastola moja aina ya bereta namba yake ikiwa imefutwa ikiwa na risasi moja, risasi tatu za bunduki aina ya shortgun, fungua 26 za aina mbalimbali na mordem moja ya kampuni ya Airtel.


Aidha kamanda huyo aliendela kusema kuwa jeshi la polisi limekuwa likimtafuta jambazi huyo kwa muda mrefu sasa tangu mwaka 2012 kutokana  na kuwahi  kutuhumiwa kushiriki katika masula ya unyan'anyi wa kutumia silaha. Jambazi huyo anahusishwa na matukio mbalimbali ikiwemo tukio la tarehe 26/08/2012 ambapo jambazi huyo akiwa na wenzake walipora bastola yenye namba T0620-11J00491 aina ya TISAS pamoja na tukio lingine la tarehe 29/08/2012 ambapo mtu mmoja aliripotiwa kuuawa,  katika tukio hilo jambazi huyo alifanikiwa kutoroka licha ya kujeruhiwa miguuni na polisi.

Hata hivyo taarifa kutoka eneo la tukio zimebainisha kuwa mmiliki wa nyumba aliyokuwa anaishi jambazi huyo anafahamika kwa jina la Swalehe ( baba Amiri). Poilisi bado wanaendele na msako ili kuhakikisha wanamkamata Salehe kwa mahojiano zaidi. (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top