Njia mojawapo nzuri katika harakati za kupambana na umaskini kwa nchi za Afrika ni kuungana pamoja katika nyanja mbalimbali za maisha hususani  nyanja ya kiuchumi.

Nazipongeza nchi za Afrika Mashariki kwa kugundua hili na kuamua kujiunga pamoja na kuunda Jumuia ya Afrika Mashariki.

Hivi sasa Baada ya jumuia hii kudumu kwa muda mrefu ikiwa imeundwa na nchi ya Tanzania, Kenya na Uganda, kwa  sasa jumuia hii imefanikiwa kupanua wigo wake zaidi baada ya nchi ya Rwanda na Burundi kujiunga.

Hata hivyo; licha jumuia hii kuoneka kuwa na manufaa mengi kwa nchi za  ukanda wa Afrika Mashariki,  jumuia hii inakabiliwa sana na chngamoto ya RUSHWA amabayo imekuwa gumzo kwa nchi wanchama wa jumuia hii 

Kwa mujibu wa gazeti la New Times la Rwanda, Uganda na Tanzania zimeonekana kuwa na kiwango kikubwa cha RUSHWA ukilinganisha na Rwanda, Kenya  na Burundi kwa mujibu wa uchunguzi ulifanywa mwaka 2012.

photo
Chati ikionyesha kiwango cha rushwa kwa nchi wanachama wa Afrika Mashariki.
Akizungumza kwenye mkutano wa kujadili namna ya kupunguza ama kuondoa RUSHWA kwa nchi wanachama wa Afrika Mashariki  uliofanyika huko Kigali Ruanda, spika wa bunge, Rose Mukantabana amesema juhudi za  nchi za Afrika Masharariki kupambana dhidi ya RUSHWA ndiyo mbinu pekee ya kuboresha jumuia ya Afrika Mashariki. (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top