Dar es salaam.

Ligi ya 'MWENYEKITI  CUP' [Bw.SULEIMAN AKIDA] 2013 kata ya Mikocheni  imeendelea kutimua vumbi lake kwa mara nyingine tena leo hii ambapo timu ya Mkunguni FC imefanikiwa kuibana mbavu Real Madrid FC kwa kuichapa   magoli 3-1





Timu ya Real Madrid ndiyo ilikuwa ya kwanza kufumania nyavu ya mwenzake mnamo dakika ya 21 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo kupitia mshambuliaji machachari "Tege Saimon" akipokea pasi nzuri kutoka kwa Janka kabla bao hilo halijasawazishwa na Mkunguni FC kupitia mshambuliaji wao anayefahamika kwa jina la Bakari mnamo dakika ya 34 ya kipindi cha kwanza ya mtanange huo.


Mchezaji wa Mkunguni FC akijaribu kupiga 'cross'
Katika mchezo huo Mkunguni Fc ilionekana kutawala mchezo kwa muda mrefu; huku wakicheza mpira makini na wa ushirikiano ambapo mnamo dakika ya 42 walipata goli la pili lilfungwa na mshambuliaji wao anayefahamika kwa jina la "Mbwana" kutokana uzembe wa mabeki wa R.Madrid ambao kwa muda mwingi wameonekana kukosa mawasiliano miongoni mwao

Kama ilivyo kawaida  ya msemo wa kiswahili usemao 'mwenye nayo huongezewa', Mkunguni FC ilipata goli la tatu na la ushindi mnamo dakika ya 69 ya mtanange huo kupitia mshambuliiaji wao aliyefunga goli la kwanza anayefahamika kwa jina la "Bakari"
Pichani hapo juu(jezi ya blue na nyeusi) ni kikosi cha Mkunguni FC.

Pichani hapo juu(jezi nyeupe) ni kikosi cha R.Madrid
Timu zingine zinazoshiriki katika ligi hii ni; Masjid Fc, Texas Fc, Wakongwe Fc, Santiago Fc pamoja na ABC Fc.

Aidha, pamoja na ligi hizi maarufu kama ligi za mchangani ama MADONDO kuleta burudani kubwa kwa wanachi walioko jirani; ligi hizi zimeendelea kuandamwa na changamoto ya ukosefu wa fedha za kuendeshea ambapo muda mwingi vijana hutembeza kibakuli kukusanya mchango kwa ajili ya kununulia maji ya wachezaji na vitu vingine kama glucose.

EXCLUSIVE: HUU NDIO UBAO WA MATANGAZO KATIKA LIGI HII YA MWENYEKITI CUP.......MIKOCHENI 2013


Pichani ni ubao wa matangazo unaotumika kutoa taarifaa mbalimbli katika ligi hii ya Mwenyeki Cup.......Mikocheni.



(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top