Mchezaji nguli wa Manchester United, Wayne Rooney ameendelea kugonga msumari wa moto  kwenye msimamo wake wa kutaka kuihama klabu yake hiyo baada ya taarifa za kuaminika leo hii kudokeza kuwa nyota huyo amegomea mazungumzo na viongozi wa klabu wa Man U ya kutaka kuongeza kandarasi ya kumuwezesha kuendelea kukipiga klabuni hapo.
 
Wayne Rooney - Manchester United v Shakhtar Donetsk
Kutoka kulia ni Wayne Rooney akikabiliana na mchezaji wa Shaktar Donetsk, Douglas Costa kwenye michuaano ya UEFA iliyofanyika Old Trafford hivi majuzi......picha na Getty image.
Habari za Wayne Rooney kutaka kuihama klabu ya Man U zilianza mwishoni mwa msimu uliopita ambapo klabu mbalimbali kama Chelsea , Arsenal, Liverpool na PSG zilionyesha nia ya kutaka kumsajili mwana soka huyo, lakini Man U  ilitupilia mbali ofa hizo na kusisitiza kuwa Rooney hauzwi.

Kandarasi ya sasa ya Wayne Rooney na klabu ya Manchester United unatarajiwa kufikia kikomo mwishoni mwa msimu ujao.

Hata hivyo kiwango cha Rooney cha soka kwa sasa klabuni hapo katika dura ya kwanza ligi kuu nchini Uingereza kimeendelea kung’ara  sana, ambapo hadi sasa amefanikiwa kufunga magoli 9 katika michezo 13 alizocheza na kuifanya Man U kuwa katika nafasi ya 9 kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingeraza.

  Chanzo: Goal.com, 9:30 pm

 
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top