Mwenyekiti Cup ndio hiyo imeendelea kushika kasi katika dimba la siku zote 'Shule ya msingi Mikocheni A'ambapo timu mbili leo zimejitupa dimbani, yaani Wakongwe Fc dhidi ya GZ Fc
Hadi kipindi cha kwanza kinaisha, timu zote mbili zilifanikiwa kupata goli moja kwa kila timu. Wakongawe Fc ndiyo ilikuwa ya kwanza kuifumania nyavu ya mwenzio kabla bao hilo halijasawazishwa na Gz Fc kwa njia penati.
 |
Ni mwendo wa kukaba njia tu.....mwenye jezi ya kijani ni mchezaji wa Wakongwa fc na mwenye jezi ya manjano ni mchezaji wa GZ Fc. |
Baada ya dakika 90 kuisha huku timu zote zikiwa zimefungana goli moja kwa moja, mshindi alilazimika kutafutwa kwa njia ya penati kwani mchezo huu wa leo ni miongoni mwa michzo itakayo amua timu ya kuingia hatua ya nusu fainali ya ligi hii.
 |
Hayo ni mambo ya kiufundi tu katika soka! |
Kati ya penati tano zilizopigwa kwa kila timu, Wakongwe wamepata penati zote huku GZ wakpata penati nne na hatimaye kutupwa nje ya michuano.
 |
Hawa ni mashabiki wa WAKONGWE FC wakishangilia timu yao.
|
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment