Mwenyekiti CUP leo hii imeendelea kutimua kivumbi chake kwa timu mbili ( TEXAS na MASJID) kukabiliana katika dimba la kila siku la shule ya msingi ya 'MIKOCHENI A'

Mtanange huo ambao ulikuwa umetawaliwa na ufundi na nguvu nyingi kutoka kwa timu zote, umefika tamati kwa timu ya MASJID kuichapa TEXAS FC magoli 3-1


Pichani ni kikosi cha Masjid kilichomchapa mtu 3-1

Hadi timu zote zinakwenda mapumziko baada ya kipinndii cha kwanza kuisha, MASJID FC walikuwa wanaongoza mchezo kwa magoli mawili yaliyosukumizwa kimyani na MUBA pamoja naye CHRISTOPHA kwa nyakati tofauti kabla ya kupata goli la tatu mnamo dakika ya 46 ya mchezo huo.


                                                    Pichani ni kikosi cha TEXAS

Nao TEXAS hawakukata  tamaa kabisa licha ya kupigwa magoli mawili kipindi cha pili; walianza kujipanga vizuri baada ya ushauri mkubwa kutoka katika benchi la ufundi na hatimaye kuweza kufunga goli moja la kufutia machozi mnao dakika ya 49 ya mchezo huo kupitia  mshambuliaji, DIKY KYUT.
 
EXCLUSIVE; MATOKEO YA MECHI ZA LEO, MAJUU.
                         Everton 2-1 Southampton
                         Newcastle united 0-1 Arsenal
                         Chelsea 2-1 Liverpool
                         Tottenham hotspurs 3-0Stock City
 
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top