Ulikuwa ni mtanange wa vuta ni kuvute kati ya vija damu changa kabisa 'ABC fc' na Santigo fc katika dimba la shule ya msingi  Mikocheni A ambapo ABC fc wamefanikiwa kuibuka kidedea kwa njia ya penati.

Hadi mtanange huo unafika dakika 90, ABC fc  walikuwa wanaongoza kwa goli moja lilotupiwa kimyani na mshambuliaji Filemon Nyange mnamo dakika ya 30 ya mchezo huo, goli hilo lilifanya ABC fc na Santiago Fc kulingana kwa kila kitu ( magoli & points) na hivyo timu zote kulazimika kwenda matuta

Vijana wa ABC fc wakitokaka uwanjani baada kusali dua baada ya kipindi cha kwanza kuisha , ABC fc  ni vijana wanaolelewa na kituo kimoja cha kukuza vipaji vya soka hapa  Mikocheni karibu na shule ya msingi Mikocheni 'A'

Baada ya timu zote kwenda kwenye matuta, ABC fc walifanikiwa kuapata penati 7 dhidi ya Santigo waliopata penati 6 baada ya penati yao moja kutolewa nje na mlinda lango wa ABC kiufundi kabisa.

Pichani ni vijana wa Santigo Fc wakito nje dimba mara baada ya kipindi cha kwanza cha mtanange huo huko nyuso zao zikikosa furaha baada kuchapwa goli moja .
Mchezo huo ulikuwa ni muhimu sana kwa timu zote mbili kwani ni mchezo ambao ungemuwezesha mmoja wao kufuzu kucheza nusu fainali ya ligi hiyo, kwa maana hiyo sasa ABC fc wameshapata tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano hii.

Muhimu; video ya penati ya ushindi kwa upande wa ABC fc, na ile waliokosa Santigo ziko kwenye page ya VIDEOS........ingia kujitazamia au ku-download.








(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top