Wengi wetu tumezoea kuona foleni ndefu ya magari barabarani hususana katika hili jiji la Dar es salaam ambalo linasemekana kuwa na idadi kubwa ya watu kuliko majiji mengine hapa Tanzania, lakini leo ( Dec 25, 2013, Chrimass day) foleni hiyo imehamia katika BUTCHERY mbalimbali hapa jiji Dar kama ilivyoshuhudiwa na mwandishi mwenzangu wa habari, Atuza G.Nkurlu.
Pia, licha ya foleni hiyo katika machinjio mengi kuwa kubwa kwa siku ya leo, nayo bei ya nyama ilikuwa haikamatikia kabisa; mfano katika butchery niliyokwenda kununua nyama leo asubuhi maeneo ya Mikocheni 'A', kilo moja ya nyama ilikuwa Tsh. 7000 badala ya bei ya kawaida ya shilingi Tsh.6000
 |
Pichani hapo juu ni wananchi wakiwa katika foleni ndefu ya kunua nyama katika moja ya machinjio iliyo maeneo ya Ubungo, Dar es salaam. Picha na Atuza G.Nkurlu. |
USHAURI: Tunaomba mamlaka husika (serikali) iwe macho katika siku kama hizi kwani wananchi wanaonewa pasipokuwa na sababu ya msingi.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment