Imekuwa kawaida na mazoea kwa jamii nyingi duniani kumchukulia mwanamke kama kiumbe dhaifu. Hii siyo kwa nchi tajiri wala maskini tu kama Tanzania ambako wanawake wamekuwa wakipiga kelele kutaka haki sawa ili kuheshika kama ilivyozoeleeka kwa wanaume.
![]() |
| wanamuziki wa kundi la Pussy Riot kabla ya kusisikiliza kesi mahakamani mjini Moscow.(kushoto ni YEKATARINA SAMUTSEVICH,MARIA ALYOKHINA NA NADEZHDA TOLOKONNIKOVA).
Vitendo vya unyanyasaji na ukatili nchini Tanzania vinaweza kuwavimesababishwa nawanawake wenyewe kutojiamini na kujitoa kupambana na kile kinachojulikana kama mfumo dume ,hasa katika nchi hizi zinazoendelea ambako vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake vimejitokeza kwa asilimia nyingi zaidi kutokana na nguvu walionayo wanaume ambayo ni matokea ya mila na desturi ya jamii zao.
|
Hali imekua tofauti kwa mataifa ya wenzetu (nchi za Magharibi) wambako wanawake wamekuwa wakijitolea kupigania haki zao pamoja wanyonge na wasiojiweza kamavile wanawake wanaoteseka ,wazee,watoto, na watu masikini.
Mfano mzuri ule wa Wanawake wa bendi ya muziki ijilikanayo kama “PUSSY RIOT” Nadezhda Tolokonnikova na Maria Alyokhina na Yekaterina Samutsevich walioamua kuachana na shughuli yao ya muziki na kuingia katika ulingo wa kupigania haki za binadamu.
Wakizungumza na waandishi wa habari ijumaa iliyopita katika mkutano uliofanyika mjini Moscow wanawake hao wamesema wanatarajia kuunda kundi la kupigania haki za binadamu litakaloitwa “Right zone”.
Uamuzi wa wanawake hao kujiingiza katika ulingo wa siasa na kushughulikia haki za binadamu unakuja siku chache baada ya kuachiliwa huru kutoka kolokoloni(Mordovia camp) ambapo walifungwa miaka miwili jela tangu Agosti 2012 kwa kosa la kumkashifu Rais Putin February 2012 katika moja ya show zao.
![]() |
| PUSSY RIOT WAKIZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MKUTANO SIKU CHACHE BAADA YA KUACHILIWA HURU KUTOKA KOLOKOLONI(KUSHOTO NI NADEZHDA TOLOKONNIVA NA MARIA ALYOKHINA) |
Aidha wanawake hao pamoja na wasomi nchini Russia walikosoa hatua ya rais wa taifa la kijamaa Vladimir Putin kuwaachilia huru wanawake hao kuwa si bure bali anajaribu kujisafisha kutokana na michuano ya Olympic inayotarajiwa kufanyika msimu wa baridi nchini humo.
Pia wameahidi kuendeleza mapambano ndani ya Russuia na dunia kwa ujumla huku wakisisitiza juu ya kuachana na fani yao ya muziki ili wapate muda wa kutosha wa kuendesha harakati zao.
Credits: habarihadharani.blogspot.com
Credits: habarihadharani.blogspot.com
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});


0 comments:
Post a Comment