Wakati wabebamitutu wa kaskazini mwa
London, Arsenal Fc hapo kesho wakitaraji kuwakaribisha Cardiff City katika dimba la ‘Emirate Studium, kibabu
wa timu hiyo ‘Arsene Wenger’ amesema anasikitishwa sana na jinamizi la majeruhi
linaloiandama klabu yake hivi sasa.
![]() |
| Kibabu 'Arsene Wenger' |
Akizungumza na waandishi wa habari
mapema leo hii, Wenger amebainisha kuwa katika mchezo wao wa kesho (Mwaka mpya
day) dhidi ya Cardiff City pale dimbani Emirate, mshamuliaji Oliver Geroud
hatakuwa miongoni mwa wanandinga kumi na mmoja watakao shuka dimbani kuikabili
Cardiff kutokana na maumivu ya ‘angle’
yanayomuandama kwa sasa
![]() |
| Oliver Giroud.
Mbali na kukoseka kwa Giroud katika
mchezo wa kesho, wanandinga wengine kama vile Mesuit Ozil,T.walcott, Tomas
Rosicky, Jack Wilshere,Kieran Gibbs,
Nacho Monreal,Tomas Vermaelen pamoja nayeAaron Ramsey hawana uhakika wa
kucheza katika mchezo huo kutokana na kukabiliwa na maumivu mbalimbali.
|
Wenger, ambaye klabu yake kwa sasa
iko kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza, ameendelea kuzungumza na
kusema kuwa katika mchezo wa kesho ana mategemeo makubwa ya kumwanzisha, Lukas
Podolski au Nicklas Bendtner ikiwa ni mbinu za kujaribu kutafuta pointi tatu
muhimu katika mchezo wa kesho.
Aidha, Wenger alipoulizwa kuhusu
tetesi za kujaribuu bahati ya kumsajili mtukutu Luis Suarez
kwa mara nyingine tena katika
dirisha dogo la usaji siku chache baadaye, baada ofa yao ya mwanzo ya £40,000,001 kugonga mwamba, alisema hawana mpango huo kwa
sasa isipokuwa wako tayari kufanya usajili wowote mwingene lakini kwa sababu maalumu.
Chanzo: Daily Mail


0 comments:
Post a Comment