Naibu katibu mkuu wa
zamani wa FIFA, bwana Jerome Champagne ametangaza kugombea nafasi ya Uraisi
wa FIFA katika uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika mwaka 2015
Jerome Champagne mwenye umri wa miaka 55 alijiunga
na shirikisho la mpira wa miguu FIFA mwaka 1999 na kufanikiwa kufanya kazi na rais
wa sasa wa FIFA ,Bw. Sepp Batter akiwa
kama naibu katibu mkuu tangu mwaka 2002 hadi mwaka 2005 na baadaye kustaafu nafasi hiyo akabaki kama mshauri wa kimataifa wa masuala ya soka
![]() |
Jerome Champagne |
Aidha, Champagne
ameendelea kusisitiza kuwa, kwa muda wa miaka 11 aliyo huudumu ndani ya FIFA
amebahatika kujifunza vitu vingi kutoka
kwa watu wenye uwezo mkubwa katika masuala ya soka hivyo anaamini yeye ni mtu
sahihi kabisa kuridhi mikoba ya Blatter.
NB: Blatter alipata urais wa FIFA mwaka 1998 kutoka kwa
Joao Havelange……….ametangaza kugombea kwa mara nyingine tena 2015
chanzo: daily mirror
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment