Mourinho amevutiwa na mshambuliaji huyo baada ya kuonyesha kiwango maridadi wakati 'The blues walipo kutana na Fc Basle kwenye michuanao ya UEFA miezi michache iliyopita msimu huu ambapo Salaha alifanikiwa kufumania nyavu mara mbili katika michezo miwili tofauti.
![]() |
Pichani ni Mohamed Salaha |
Miongoni mwa klabu vilivyokuwa vinamuwinda Salaha ni Majogoo wa London Liverpool lakini mkono wao wa birika umewaponza mpaka Chelsea wamechangamkia dili hilo na hatimaye kufanikiwa kumsainisha mshambuliaji huyo.
Lakini huko Man U bado hali siyo shwari kwani meneja wa Rooney, Paul Stret Stretford bado anaendelea kukomaa kutaka uhamisho wa mshambuliaji huyo ambaye hivi karibuni amekuwa akitakiwa na vilabu tofauti ikiwemo Real Madrid na Chelsea.
Hapo jana meneja wa Rooney Paul alionekana katika uwanja wa mazoezi wa Man U ulioko mjini Carrington akijaribu kuangalia maendeleo ya mchezaji wake kabla ya kurudi leo huko mitaa ya Oldtraford kuonana na mtendaji mkuu wa klabu ya Man U Bw. Ed Woodward kwa ajili ya kuzungumzia kama Rooney atakubali kusaini kandarasi mpya klabuni hapo.
Chanzo: The Daily Mail. (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment