Mtanange wa kesho kati ya Majogoo wa London, Liverpool dhidi Fulham umeingiwa na wasiwasi wa kutochezwa kwa sababu ya mgomo wa magari moshi (treni) unaoendelea pale jijini London.

Strike: London Underground workers staged a 48-hour walkout last week, and another is planned this week
Pichani ni wafankazi wa shirika la reli jijini London wakiwa katika mgomo.
Kutokana na hali hiyo mmliki wa  klabu ya Liverpool John W. Henry amevunja ukimya kusema kuwa atashangazwa mno na klabu ya Fulham endepo itaamua kuhairisha mchezo huo unaotarajiwa kufanyika kesho katika  dimba la Craven Cottage jijini London eti kwa sababu ya mgomo huo wakati mechi zingine kati ya Arsenal na Manchester United wenyewe utaendelea kama kawaida.

Klabu ya Fulhamu kwa upande wao wanadai kuwa mgomo huo utawafanya viongozi wengi wa klabu hiyo wanaotegemea usafiri wa treni kushindwa kufika uwanjani, lakini wamesisitiza kuwa hadi kufika saa 12:00pm (Juma nne) leo  mchana kwa saa za Afrika Mashariki watakuwa wamejua kama mchezo huo utachezwa ama hautachezwa.
In doubt: Fulham's match with Liverpool on Wednesday could be called off due to the Tube strike
                                     Makao makuu ya klabu ya Fulham

Kwa mujibu Website ya THE GUNNERS, wao wanaombea mchezo huo uchezwe kwani isipo chezwa kesho, wapinzani wao 'Liverpool' ambao juzi  waliwafanyia kitu kibaya cha magoli matano kwa moja watakuwa wamepata muda mwingi wa kupumzika. Arsenal wanatarajia kucheza na Liverpool jumapili ijayo.

Credits; Daily mail. (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top