Baada ya
mtanange wa jana kati ya Arsenal na bingwa
mtetezi wa ligi kuu nchini Uingereza Manchester United , Meneja wa ArseanaL
Arsene Wenger amesema amesononeshwa sana na matokeo ya hayo ya kutofungana dhindi ya bingwa huyo katika dimba la nyumbani,
Fly Emirates.
Akiongea na
vyombo mbalimbali vya habari, Wenger amesema walikuwa na kila sababu ya kuibuka
na ushindi katika mchezo huo dhidi ya Mashetani wekundu, lakini safu yake ya
ushambuliaji iliyokuwa inaongozwa Oliver Geroud haikuwa makini sawasawa katika
eneo la hatari, lakini amesema bado anawashukuru vijana wake kwa kutoruhusu
ngome yao kuguswa
![]() |
| Arsene Wenger |
Hata hivyo
Arsenal baada ya hivi juzi kutoka kupigwa magoli 5-1 na Liverpool katika
michuano ya ligi kuu nchini Uingereza, sasa wanajiandaa kuwapokea Liverpool
Juma pili ijayo katika michuano ya FA.
Tukiachana
na habari hiyo tuelekee huko nchini Hispania ambapo miamba ya soka nchi himo Barselona Fc na Real Madrid
wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya
michuano ya Copa Del Rey ama kwa lugha ya Kiswahili, kombe la mfalme
itakayochezwa Aprili 16 mwaka huu.

Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia baada ya ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Atiletical Madrid.
Real Madrid ndiyo walikuwa wakwanza kujihakikishia nafasi hiyo ya kucheza fainali ya kombe la mfalme baada ya kuwatandika mahasimu wao Atiletical Madrid magoli mawili kwa sifuri, magoli ambayo yalifungwa na nyota wa soka duniani kwa sasa , Cristiano Ronaldo kwa mikwaju ya penati
Nao Barcelona
ambao ni wapinzani wakubwa wa Real Madri
huko nchi Hispania hapo jana wameweza
kujihakikishia nafasi kucheza fainali hiyo baada ya kutoka sare ya goli moja kwa moja dhidi ya
Real sociedal.

Mesi(kulia) akifanya mambo yake wakati wa mechi yao dhidi ya Real sociedal, mchezo huo ulimalizika kwa sare ya goli 1-1
Fainali hiyo
ya tarehe kumi na sita mwezi wa nne mwaka huu kati ya Barcelona na Real Madrid itakuwa ni ya fainali ya saba kihistoria
katika kombe hili la mfalme,ambapo fainali ya kwanza iliyowahi kuwakutanisha
wababe hawa wa ligi kuu ya Hispania ilichezwa mwaka 1936 mwezi mmoja tu kabla
ya kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe vya nchini Hispania maarufu kama Spanish Civil War.
Fainali hiyo
ilifanyika katika dimba la a Mestella ambapo Real Madrid walifanikiwakuibana
mbavu Barcelona kwa kuifunga magoli 2-1 na kuondoka na kombe.
Fainali ya
hivi karibu ya kombe la Copa De Rey iliyowakutanisha Barcelona na Real Madrid
ilkuwa fainali ya mwaka 2011 ambapo Real Madrid waaliibuka mshindi baada ya kuifunga Barcelona goli moja kwa sifuri.
credits; Goal.com
credits; Goal.com

0 comments:
Post a Comment