Wakati bingwa mtetezi wa kombe la ligi kuu nchini Uingereza, Manchester United wanajianda kuwakabili Aston Villa katika dimba lao la nyumbani Old Trafford, Mashabiki wa timu hiyo wamekodi ndege itakayo peperusha angani bango kubwa linalo mshinikiza kocha mkuu wa klabu hiyo Davidi William Moyes kubwaga manyanga.

Moyes out banner
Pichani ni ndege inayotarajiwa kupeperusha angani bango kabla ya mechi ya leo dhidi ya Aston Villa linalomtaka Moyes abwage manyanga.

Hatua hii imefikiwa na mashabiki wa Red Devils baada ya klabu yao kuendelea kuandamwa na matokeo mabaya chini ya uongozi wa Moyes tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita wakati timu hiyo ikiwa chini ya Sir Alex Furguson.

Ama kwa hakika msimu huu, Manchester united imejikuta ikivunja rekodi mbalimbali kwa kuruhusu kufungwa na timu ndogo wakati huohuo ikiwa kibonde kwa timu kubwa za Uingereza kama vile Liverpool, Manchester City na Chelsea kwa kuwataja wachache.

Hata hivyo licha ya mashabiki kote ulimwenguni kumshutumu Davidi Moyes kuwa hana uwezo wa kukinoa klabu ya Man U, yeye binafsi kupitia gazeti la Daily Mail amesema kuwa hata ingekuwa ni Furguson ndiye anayefundisha klabu hiyo kwa sasa bado asingekuwa na cha kufanya zaidi ya anachokifanya yeye klabuni hapo.

All change: Moyes took over at United in the summer but has struggled to inspire his team
David William Moyes
''Hata kama ingekuwa ni Sir Alex Furguson ndio yuko hapa msimu huu  bado mambo yangekuwa magumu kwake pia kama ilivyokuwa  kwangu leo, naamini atakubaliana na mimi kwa hili'' Moyes alisema .


(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top