Baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo, timu ya School of journalism and Masscommunication (SJMC Fc)  hapo jana imefanikiwa kuicharaza timu ya College of Information and Communication Technology (COICT  Fc) kwa magoli 5-0 katika mchezo uliofanyika uwanja wa main campus chuoni hapo.

Hadi timu zote zinakwenda mapumzikoni, timu ya SJMC ilikuwa inaongoza kwa goli moja kwa sifuri, goli lilofungwa na mshambulia hatari wa kushoto Brayan Oviedo mnamo dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza.

Nyanda wa COICT akijaribu kuokoa goli la kwanza liliofungwa na SJMC kupitia mshambuliaji Oviedo
Beki wa COICT Fc akiondoa mpira katika eneo la hatari.
Baada ya timu zote kurudi uwanjani kumalizia ungwe ya mwisho ya lala salama, COICT walionekana kulemewa kwa kiasi kikuwa hasa katika idara ya kiungo na ushambuliaji na hatimaya kuweza kuruhusu magoli mengine manne na kuifanya mchezo huo kumalizika kwa SJMC kuibuka na ushindi wa magoli matano kwa sifuri.
kushoto ni mshmbuliaji wa SJMC OVIEDO  akijaribu kumtoka beki wa COICT
Hata hivyo SJMC bado ilikuwa na uwezo wa kushinda magoli mengi zaidi katika mchezo kutoka na kutengeza nafasi nyingi za wazi, lakini mshambuli wa mbele Peter Mabere maarufu kwa jina la BOKO alikuwa kikwazo kwani ndiye aliyepata nafasi nyingi za kufunga lakini alishindwa kufanya hivyo kabisa na hatimaye kocha mkuu wa timu hiyo Francis Kivuyo kulazimika kumtoa nje huku nafasi yake ikichukuliwa na supersub Reyson.
Kushoto ni mshambuliaji wa SJMC Peter Mabere akimpisha Reyson baada ya kuonyesha kiwango kibovu kabisa uwanjani hapo.


Ushindi huo umewafanya mashabiki wa SJMC Fc kufufuka kwa mara nyingine tena baada wachache wao kuanza  kuonyesha hali ya  usaliti baada ya timu hiyo kula kipigo kizito katika mechi mbili za mwanzoni ambapo mechi ya kwanza dhidi ya SOED Fc  March 23, 2014 walipigwa 8-0, wakati mechi ya pili dhidi ya CASS March 26, 2014 walikula 4-1.
Mashabiki na wachezaji wa SJMC wakishangilia ushindi huo wa magoli 5-0 dhidi ya COICT.
Ili kuingia katika hatua ya robo fainali, SJMC Fc sasa wanatakiwa kushinda siyo chini ya magoli 6-0 katika mechi ijayo dhidi ya kitivo cha kiswahili (IKS ) itakayo pigwa katika dimba la main campus.

Muhimu: Picha zote na Atuza G. Nkurlu



(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top