Maelfu ya watoto nchini Uingereza na Wales, wanakabiliwa na tisho la kukosa elimu huku walimu wao wakigoma.
![]() |
| Pichani ni walimu nchini Uingereza wakiwa katika mgomo. |
Walimu hao wanagoma wakitaka nyongeza ya mishahara, malipo mazuri ya uzeeni na kuboreshwa kwa mazingira ya kazi.
Walimu hao wamesema hawakuwa na budi ila kuondoka kazini kwani hakuna suluhu la matatizo yao.Wanachama wa chama cha walimu, (NUT) watashiriki katika mgomo huo huku wakiacha shule nyingi bila walimu huku masomo yakisitishwa.
Wizara ya elimu hata hivyo imelalamika ikisema kuwa mgomo huo unaathiri maisha ya wazazi na elimu kwa watoto.
Mgomo huu ulianza baada ya walimu kukubaliana kupiga kura ya kugoma au kutogoma mwezi Mei 2011 na Juni 2012 ambapo asilimia 92 ya walimu walipiga kura ya ndio mgomo ufanyike.
Chama cha walimu nchini humo kimekuwa kikivutana na serikali kwa miaka miwili sasa na hata kufanya migomo midogomidogo hadi mgomo huu mkubwa ukafikiwa.
Chanzo: bbc
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:
Post a Comment