Bingwa mtetezi wa Baclays Premier league 2013/2014 Manchester City wamepigwa faini ya € milioni 60 UEFA baada ya kugundulika kuvunja sheria za Financial Fair Play (FFP)
Mara baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi kuu ya Uingereza May 11 mwaka huu kwa Man city kutawazwa bingwa mpya, klabu hiyo imesoma mapato na matumizi na kujikuta ikiingia hasara ya zaidi ya € milioni 30 hasara ya wastan inayo kubaliwa na UEFA.
Man City imeingia hasara hiyo ambayo wao wenyewe hawakuweka wazi kuwa ni hasara ya kiasi gani, kwa kuwekeza zaidi katika maadandalizi ya michuano hiyo ambayo hata hivyo walitolewa katika hatua ya robo fainali na Barcelona.
Mbali na adhabu hiyo,Man City pia wamepigwa adhabu ya kupungunza wachezaji katika kikosi chake hadi kufikia wachezaji 21 totauti na idadi ya wachezaji 25 wanaoruhusiwa na UEFA kuelekea michuano ya UEFA 2014/2015.
credits: ESPN.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment