Wana familia hao wanao patikana katika mitaa ya Xibianban kusini mwa China wameamua kuchukua hatua hiyo ngumu kwa mwanao ili kujaribu kudhibiti tabia yake ya wizi kwani wasipo fanya hivyo wanaamini muda siyo mrefu kijana huyo atakuwa magereza
![]() |
Chuang akiwa amelala chumbani kwake huku akiwa amefungwa cheni shingoni |
Aidha mzee Wen Yuan ameendelea kusema kuwa mara kwa mara amekuwa akilipa vitu alivyo viiba mtoto wake kwa majirani huku akilazimika pia kuwaomba msamaha kwa tabia hiyo ya mwanae na sasa amechoka kulipa hasara hizo hivyo ameona kilichobaki kwa mwanae ni kumfungia ndani ya chumba chake cha kulala kwa kutumia cheni.
![]() |
Chuang (haonekani katika picha) akiwa ametoka kidogo upande mwingine wa chumba chake. |
Chuang amefungiwa katika chumba chake cha kulala kwa kutumia cheni ndefu ambayo itamuwezesha tu kuzunguka humo ndani na siyo vinginevyo.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment