Mmiliki wa klabu ya  Manchester United, Malcolm Glazer ameripotiwa kufariki dunia leo hii akiwa na umri wa miaka 86
Malcolm Glazer

Mbilionea huyu kutoka Marekani aliinunua Manchester United tangu mwaka 2005 kwa gharama ya Uro milioni 790 licha ya mashabiki wa klabu klabu hiyo kumpinga vikali kipindi hicho.

Ikiwa chini ya mikono yake, The Red Devils wamefanikiwa kuchukua vikombe vitano vya ligi kuu nchini Uingereza, EPL-2005,2008,2009,2011,2013 pamoja na UEFA 2008.

Pamoja na hayo, kifo hicho kinasemekana kuto adhiri umiliki wake wa klabu hiyo kwa sababu ana hisa kubwa mno klabuni hapo inayofikia asilimia 90.


credits: dailymail.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top