Michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U-20)  yanayofahamika kwa jina la Rolling Stone kwa mwaka 2014 yamefikia tamati leo July 28, 2014 kwa Azam Fc kuibuka  bingwa mpya wa michuano hiyo baada ya kuinyuka Twalipo Fc magoli 2-0 katika kipute kilichopigwa katika dimba la Karume jijini Dar es salaam majira ya jioni.


Displaying IMG_20140728_180713.jpg
Displaying IMG_20140728_180757.jpg
Azam FC  U-20 wakifurahia ubingwa wa Rolling Stone ya mwaka 2014 yalifanya katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam July 28,2014.


Mshambuliaji wa Azam (jezi nyeusi) akijaribu kumtoka beki wa Twalipo Fc
Katika kipute hicho ambacho kilikuwa cha kusisimua zaidi, Azm Fc ndiyo ilikuwa ya kwanza kufumania nyavu ya wenzao kupitia mshambuliaji wao machachari, Jamir Mchaulo mnamo dakika ya 3 ya mtanange huo kabla ya Adam Sota kusukumiza goli lingine la pili na lililopoteza kabisa matumaini ya Twalipo Fc dakika ya 85 ya kipute hicho.


Akiteta na  mtandao huu katika uwanja wa Karume, kocha mkuu wa Azam Fc-U 20, Viveck Nagul amesema, siri ya mafinikio ya ushindi wao katika mchezo huo ni wao kuwekeza kwa bidii katika ujenzi wa timu yao bila kuogopa gharama.

Kikosi cha Azam FC U-20 kilichotwaa ubinwa.

"Ukijaribu kuangalia katika michuano hii tangu yalipo anza wiki mbili zilizopita, Azam FC tulianza vizuri, tulikuwa tunashinda kwa magoli mengi, kwa hiyo kwa muonekana huo utagundua kabisa sisi tulikuwa ni timu nzuri na ngumu kwa wapinzani wetu kwa sababu tumetumia gharama nyingi kuandaa kikosi chetu".Alisema Viveck Nagul.


kocha mkuu wa Azam Fc U-20 Viveck Nagul, akiwa makini kuangalia vijana wake wanafanya nini uwanjani.

Lakini kwa Upande wake Kocha wa Timu ya Twalipo Fc, Ally Shabani, alisema pamoja na kuwa michezo hii ni muhimu kwa vijana wetu ilikuwa haifuati baadhi ya kanuni za mashindano na ndo sababu timu yake iliweza kupoteza mchezo huo kwa kuchezea kichapo cha magoli 2-0.

Kikosi cha Twalipo Fc kilichokuwa kikikabiliana na Azam Fc

"kwangu mimi naweza kusema mashindano kwa kweli hayakuwa mazuri wala mabaya, haiwezekani timu zinacheza kila siku mfululizo bila kupata muda wa kupumzika, huo utaratibu kwa kweli haujawahi kuonekana duniani isipokuwa katika mashindano haya Rolling Stone ya mwaka huu"

Wa kwanza kutoka kulia (jezi ya blue) ni kocha mkuu wa Twalipo FC, Ally Shabani akiwa na Benji lake la ufundi.
Aidha, mmoja kati ya wanakamati waliohusika kuandaa michuano hiyo, kocha wa timu ya Combine ya Shinyanga, John William "kocha Delipielo" ambaye pia ni mkuu wa waamuzi mkoa wa Geita, alisema michuano yalifaana sana kwa sababu wao walitegemea kupokea timu 20 lakini walipokea timu 32 tofauti na matarajio yao.

Mbali na hilo, William pia alizungumzia changamoto ambazo ziliweza kuonekana katika michuano hiyo, machache kati ya hizo yakiwa na ni udanganyifu wa umri kwa wachezaji pamoja na ukosefu wa wadhamini wa kutosha.

"Changamoto kubwa ilikuwa ni kwenye suala la umri, bado wachezaji  wanadangnya umri, ukijaribu kuangalia hapa kuna baadhi ya wachezaji ukiwaangalia kwa muonekano wao wa nje, unapata shaka  kwamba huyu siyo U-20 kabisa", William alisema.

Hata hivyo, makocha wa klabu mbalimbali hapa nchini walikuwepo katika fainali hizo wakijaribu kuangalia vipaji ambavyo wangeweza kuwasajili kwa mipango ya ujenzi wa timu zao za U-20 kwa faida ya baadaye.

Kocha wa Dar Young Africans, Mbrazil, Marcio Maximo, alikuwa ni miongoni mwa makocha wa timu kubwa za hapa nchini aliyekuwa katika uwanja wa Karume kuangalia vipaji ambazo ataweza kuvitumia katika timu ya klabu hiyo ya U-20.

Pichani ni kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Marcio Maximo akiwa uwanja wa Karume kufuatilia mashindano ya Rolling Stone ya mwaka 2014, Maximo pia alikuwa kivutio kwa baadhi ya mashabiki hususani watoto waliokuwa uwanjani hapo

Akilonga na mtandao huu, uwanja wa Karume, Maximo alisema kupitia michuano hiyo ya Rolling Stone, ameona kuna vipaji vingi ambavyo vikitunzwa vitakuwa ni hazina kubwa kwa taifa katika tasnia ya soka la Tanzania.

Marcio Maximo akiteta jambo na kocha wa  Yanga wa timu ya vijana U-20, Salvatory Edward, Uwanja wa Karume leo katika mashindano ya Rollingi Stone
"Nachoweza kusema ni kwamba hapa Tanzania kuna  vipaji halisi vya soka, kikubwa ni kupata muda wa kuwafundisha vijana hawa zaidi....I can compare these players with Diamond, you know, inorder to get a good dimond you need to polish it". Maximo alisema.







(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});

0 comments:

Post a Comment

 
Top