1.Matumizi ya spray(kinyunyizio)
Baada ya matumizi yake kuonyesha msaada mkubwa katika michuano ya WC 2014 huko nchini Brazil, kifaa hiki sasa kimekwisha dhibitishwa kutumika na waamuzi katika ligi kuu ya Uingereza.
Pichani ni refa akionyesha matumizi ya kinyunyizio uwanjani. |
2.Kupanda kwa gharama za tiketi za kuingilia uwanjani kwa msimu mzima 2014/2015 .
Arsenal FC ndiyo klabu ya kwanza ya EPL kwa sasa kutangaza kupanda kwa gharama za tiketi za kuingilia uwanjani kwa msimu mzima ujao, ghama zao zitakuwa ni zaidi ya paundi 2,000 tofauti na misimu iliyopita.

3.Ujio wa makocha wapya (Louis Van Gaal aka Mr....3:5:2)
Moja ya vitu vinazungumzwa sana kuhuzu ligi kuu ya Uingereza ni pamoja na ujio wa kocha mpya katika klabu ya MAN U, Louis Vana Gaal, hii ni kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kufundisha soka.
Makocha wengini wapya wanaozungumziwa ni; Ronald Koeman-Southampton, Nigel Pearson-Leicester (imepanda daraja msimu huu), Sean Dyche-Burnley(imepanda daja msimu huu), pamoja na Alan Irvine-West Brom.
Louis Van Gaal. |
4.Mpira utakaotumika.
'Nike Ordem' ndiyo aina ya mpira utakaotumika katika EPL msimu unaokuja Agost 16, 2014. Mpira huo unasifika kwa kuwa na mvirongo mzuri, lakini pia ikiwa na rangi nzuri zinazofanya ionekane kwa urahisi.
Mpira aina ya Nike Ordem |
Baada ya kustaafu kupuliiza kipenga, sasa webu atakuwa akionekana BBC, SKY na BT akichambua maamuzi yatakayokuwa yakifanywa na waamuzi mbalimbali.
Howard Melton Webb. |
Katika kila mechi ya EPL, kutakuwa na daktari wa kutoa maamuzi kama mchezaji aliyepata majeraha ya kichwa ataendelea kucheza au atatoka nje.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment