Makala.....
Tanzania ni nchi
mojawapo duniani inayojihusisha kwa
kiasi kikibwa na masuala ya michezo kama sehemu ya burudani lakini pia kama sehemu ya ajira kwa vijana,
ingawaje katika kipengele cha ajira bado haijafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Kama ilivyo kwa nchi zingine, Tanzania imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kukuza, kuboresha na kuendeleza mchezo wa soka. Miongoni mwa jitihada hizo ni kuazisha au kuruhusu mashindano mbalimbali ya vijana wenye umri tofautitofauti kufanyika, mfano mashindano ya Aitel Rising Stars pamoja Rolling Stone kwa kutaja chache tu.
Katika maka hii, leo
tunaangalia zaidi mashindano ya Airtel Rising Stars ambayo yameanzishwa na
kampuni ya Airtel inayojihusisha na utengenezaji
na uuzaji wa laini za Airtel hapa nchini.
Programu ya Airtel
Rising Stars ambayo hadi sasa imefanyika kwa mara ya nne hapa nchini tangu
ianzishwe,ilikuwa na lengo moja kubwa tu
ambalo ni kuibua vipaji vipya vya soka la wanaume na wanawake wenye umri chini
ya miaka 17 kutoka mitaani, kisha klabu na vituo mbalimbali vya soka vya hapa
nchini kupata fursa ya kujipatia wachezaji wapya kiurahisi kwa ajili ya timu
zao.Cha ajabu na cha kusikitisha ni kwamba lengo la programu hii ya Airel Rising Stars la kuibua vipaji vipya vya soka nchini, linapotoshwa na watu wachache wanaojifanya kwamba wao hawaelewi lengo la program hii kwa kuwachezesha wachezaji ambao tayari wamesha ibuliwa siku nyingi misimu iliyopita na tayari wana klabu zao wanazochezea.
Nasema hivyo kwa sababu nilikuwa nikufuatilia kwa ukaribu mashindano haya ya Aitel Rising Stars msimu wa 2014 tangu yalipo anza na hatimaye kufikia tamati hapo jana Agost 17,2014 katika uwa wa kumbukumbu wa Karume ndipo nikagundua kwamba kupata vipaji vipya vya soka kupitia mashindano hayo ni ngumu kwa sababu sehemu kubwa ya wachezaji waliokuwa wanachezea timu za mikoa yao katika mashindano hayo walikuwa ni wale ambao tayari walisha ibuliwa misimu iliyopita na tayari wana klabu zao wanazochezea kwa sasa, wachezaji wapya ni wachache mno.
Tatizo kubwa hapa ni
kwamba watu wamekuwa wakitanguliza mbele maslahi yao binafsi kuliko kujali
lengo la mashindano yenyewe, kwa maana ya kwamba wanajali zaidi kuchukua
ubingwa na kisha kunufaika na zawadi watakazo pewa mara baada ya ubingwa huo na
ndiyo maana wanalazimika kuwachezesha wachezaji
wale wale wa misimu iliyopita ili kuhakikisha wanachukua ubingwa. Huu ni
ukosefu wa maadili!
Ubabaishaji huu siyo kwamba
tu unawanyima wachezaji wapya fursa ya kuonyesha
vipaji vyao, bali pia itawakatisha tamaa waandaaji wa mashindano yenyewe na
mwisho wa siku wataamua kukaa pembeni na ndipo sasa tutakapo anza kumtafuta
mchawi ni nani wakati ni sisi wenyewe.
Ni wazi kwamba ili
Tanzania iweze kuendele kisoka, njia pekee ni kuwekeza kwa vijana wadogo
kuanzia ngazi ya chini kabisa (mitaani)
kama ambavyo Airtel wameanza kufanya, kwa sababu mchezaji mzuri ni yule
anayekulia katika mpira kwani anakuwa amekomaa kimaadili lakini pia anakuwa na
ufahamu wa awali wa soka na hata atakapo kuwa mchezaji mkubwa anakuwa
anafundiahikia kirahisi.
Fuatilia nchi
zilizoendelea kisoka iwe Afrika au Ulaya, utagundua kabisa kwamba wana mikakati
mizuri tena ya muda mrefu na wanajitahidi kusimamia kikamilifu mikakati yao,
mfano mzuri ni Ujeruma ambao hadi kufikia mwaka 2000 karibu kila kitongoji kuna
football academy na matunda yake yameanza kuonekana,na ndiyo maana mwaka huu tumeshuhudia Ujerumani ikitwaa ubingwa wa kombe la dunia
huki kikosi chao kikiwa kimesheheheni vijana damu changa, mfano
mshambuliaji Julian Draxler 20
anayekipiga kunako kunako klabu ya Schalke 04 ya nchini humo.
Kabla ya Mashindano ya
Aitel Rising Stars kuanza, Mwezi July mwaka huu kulikuwa na mashindano mengine
ya Rollingstone ambayo kimsingi yalikuwa
na lengo sawa na lile la Aritel Rising Stars ambapo nilipata nafasi ya kutete
kidogo na kocha mkuu wa klabu ya Dar es salaam Young Aficans, mbrazil, Marcio
Maximo ambaye alikuwa katika uwanja wa Karume kufuatilia kwa ukaribu mashindano
hayo na alikiri mwenyewe kwamba Tanzania tuna vipaji asilia vya soka ila
kinachohitajika kwa sasa kwa vijana wetu ni kupatikana kwa muda wa kurekebisha mambo madogo madogo.“Tanzania kuna vipaji vingi sana vya soka, nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu mashindano ya Rolling Stone tangu yalipoanza, na kwa kweli mimi mwenyewe nimeshangaa kuone uwezo mkubwa unaoonyeshwa na vijana hawa. Nachoweza kusema ni kwamba wanachohitaji hawa vijana kwa sasa ni muda wa kurekebishiwa mambo madogo madogo na kuongezewa mashindano zaidi, kwa kufanya hivyo klabu za Tanzania zitakuwa na wachezaji wazawa wazuri sana” Maximo alisema.
Kama mashindano ya soka
la vijana nchini Tanznia litafanyika kwa kutambua malengo tuliyo nayo na kwa kufuata uaratibu uliowekwa, naamini
wadau wengi wa soka watajitokeza kutoa msaada wao wa hali na mali na mwisho wa
siku tutasonga mbele.
Haina maana yoyote
kuharibu mipango ya wengi ili kufurahisha nafsi ya mtu mmoja. Hii maana yake ni
kwamba timu ambazo zimechezesha wachezaji ambao tayari walishaibuliwa na Aitel
Rising Stars misimu iliyopita katika mashindano ya msimu huu ni wazi kwamba
wamepotosha maana na lengo halisi la mshindano yenyewe, na wana kila sababu ya
kuona haya kwa hili. Ni imani yangu na wengi pia kwamba hakuna mtu aliye tayari kuwekeza katika mambo ambayo hayana mwelekeo dhabiti, kwa hiyo ni lazima kila mtu kwa nafasi yake atimize wajibu alionao pamoja na kuwa mzalendo kwa nchi yake.
0 comments:
Post a Comment