Kiungo wa Manchester United, Maroune Fellaini atakuwa nje ya dimba kwa muda usiojulikana baada ya kupata majeraha akiwa mazoezini na klabu yake hiyo katika uwanja wao wa mazoezi, Carrington. Hii sasa ni changamoto kubwa kwa Luis Van Gaal, ambaye yuko katika harakati za kuamua nani apigwe mnada klabuni hapo ili kupata nguvu ya kufanya usajili mpya.
Fellaini ni miongoni mwa wanandinga wa Man U ambao walikuwa katika ratiba ya watakao uzwa msimu huu na tayari baadhi ya klabu kama vile Fc Napoli zilisha onyesha nia ya kumtaka Mbeligiji huyo amabye kwa hakika uwezo wake msimu uliopita haukuwa wa kuridhisha.
 |
Nje ya dimba kwa muda usiojulikana: Pichani ni Fellaini akitembea kwa magongo baada ya kupata majeraha ya ANKLE akiwa mazoezini na timu yake katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo huko Carrington.
Sasa Maroun Fellaini anakuwa kwenye orodha ndefu ya wachezaji wa Man U walioko nje ya dimba kwa sababu ya majeraha mbalimali ambao ni akina; Carrick, Jonny Evans, Danny Welbeck, Tom Cleverley, Luke Shaw pamoja na Antonio Valencia
|
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment