Huenda mchezaji wa kati wa klabu ya, Aaron Ramsey akakosa mtanange wa Jumamosi kati ya Arsenal dhidi ya bingwa mtetezi wa ligi kuu nchini Uingereza, Manchester City baada ya kupata kuripotiwa kupata jeraha la kifundo cha mguu wakati akichezea timu yake ya taifa ya WALES dhidi ya Andorra jana usiku.
Ni hatari: ni wakati mwingine mgumu kwa Arsene Wenger kueleke mchezo wake wa Jumamosi hii dhidi ya Man City endapo majeraha aliyo yapata Ramsey hayatamruhusu kuwa sehemu ya kikosi. |
Katika mchezo huo ambao ulikuwa kuwania kufuzu kushiriki mashindano ya UROPA 2016, timu ya taifa ya WALES imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-1.
Andorra ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 6 kwa njia ya penati ambayo lilifungwa na Ildefons Lema wakati magoli yote mawili ya WALES yakifungwa na Gareth Bale kwa nyakati tofauti.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment