![]() |
Hiyo ni picha inayo onyesha jinsi Wenger alivyo mfuata Mourinho na kumsukuma katika mechi ya wikiendi iliyo pita ambayo Chelsea iliibuka na ushindi wa Magoli 2-0. Wenger alifanya tukio hilo baada ya kujibizana na Mourinho juu ya rafu aliyo chezewa Alex Sanchez na beki wa Chelsea, Gary Cahill. |
"Siku zote sipendezwi na hali yoyote ya uhasama na kwa kutambua hilo, naomba msamaha kwa kitendo nilicho kifanya kwa kocha mwenzangu, Mourinho. Hali ya hasira humtokea mtu yeyote. Lakini pia ikumbukwe sikuingia katika eneo la Mourihno kama ambavyo watu wanasema"
Mpaka sasa bado shirikisho la kandanda nchini Uingereza FA, halijasema litachuakua hatua gani dhidi ya Wenger na mwenzake Mourinho.
(adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});
0 comments:
Post a Comment